Saturday, October 15, 2016

GUARDIOLA ATAKA MAKUBWA ZAIDI KUTOKA KWA KUN AGUERO

Sergio Aguer na kocha wake Pep Guardiola wakiwa mazoezini.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ametaka makubwa zaidi kutoka kwa winga wake machachari Sergio''Kun''Aguero. Ingawa Aguero ameanza msimu vizuri lakini kocha huyo bado anahitaji mazuri zaidi kutoka kwake.
 Aguero ambaye ameanza msimu kwa kiwango kikubwa akiwa chini ya kocha huyo, tayali ameshafunga mabao 11 kwenye michezo nane  kwa City msimu huu. 

Guardiola amesisitiza kwamba Muargentina huyo anaweza kufanya mazuri zaidi kwenye timu hiyo. 

''Nikisema nahitaji mengi kutoka kwa Kun sio kwamba sina furaha juu ya kiwango chake, sio kweli,'' Guardiola aliongea kuelekea mbele mechi yao dhidi ya Everton Jumamosi hii kwenye Premier League baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Akizungumzia kipindi chake alichokuwa chini ya johan Cruyff akiwa Barcelona, Guardiola alisema ''pale hawakuangalia tabia yangu kamwe, siku zote walikuwa wanakusukuma ili ufanye vizuri. 

''Pengine nimepata kitu kama hicho hata nilivyokuja kuwa kocha, kwa hilo najivunia. 

''Wanaweza kufanya vizuri, naweza nikafanya vizuri, na kila mtu anaweza kufanya vizuri, ninahitaji kuwasukuma na inawapasa kukubaliana na hilo.

Huku Muargentina huyo akiwa na kiwango kibovu kwenye timu yake ya taifa ya Agerntina hali ambayo imepelekea kupata lawama toka kwa mashabiki wa taifa hilo, lakini Guardiola alimtetea na kusema kwamba hali hiyo haimtokei Aguero peke yake bali inaweza kutokea hata kwa Messi, Di Maria(Argentina) Neymar , Dani Alves(Brazil), Rahim Sterling(England).

''Ukicheza vibaya na kupoteza mchezo, wanakuua.'' 

No comments:

Post a Comment