Wednesday, October 5, 2016

NATAMANI KURUDI UWANJANI- SHARAPOVA

 Baada ya kushinda rufaa kupinga maamuzi ya kufungiwa miaka miwili bingwa namba moja wa zamani wa mchezo wa tenisi Maria Sharapova amepunguziwa hukumu kutoka miaka miwili mpaka miezi 15.
Na sasa atarejea uwanjani April 26, 2017. 

Sharapova alionyesha shauku yake ya kutaka kurejea uwanjani baada ya kuwaambia mashabiki wake kupitia mtandao wa kijamii wa facebook, 
 ''Tenisi ni maisha yangu na nilikikosa hicho, ninarudi muda si mrefu na siwezi kuendelea kusubiri,'' alisema mcheazji huyo mwenye miaka 29. 
 Sharapova ambaye ni mshindi mara tano wa Grand Slam alikutana na adhabu hiyo baada ya kugundulika alikuwa akitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni za meldonium, na kupelekea Shirikisho la Kimataifa la Tenisi kumfungia kwa miaka miwili.
 
 

''
 

No comments:

Post a Comment