Monday, September 19, 2016

BALOTELLI ATAREJEA PREMIER LEAGUE -RAIOLA



Wakala wa mchezaji Mario Balotelli, Mino Raiola amesema kuwa mchezaji huyo atarejea Premier League kwa siku za mbeleni.

Mshambuliaji huyo wa Italia aliondoka Liverpool na kujiunga na Nice kwa usajili huru baada ya kuwa katika hali ya sintofahamu  Merseyside. 



                     Balotelli amepata matokeo mazuri na ya haraka tangu ahamie Nice.


Raiola amesisitiza kuwa ni suala la muda tu hapo kabla, lakini Balotelli mwenye miaka 26, atarejea Uingereza. 

Akiongea na Daily Mail, Raiola alisema kuwa ''hawezi kuishi Italy kwa sababu ya tahadhari anazopata. 

''Kama atathibitisha kuwa imara na bora kwa Nice na kufunga mabao, hebu fikiria jinsi atakavyo washashiwi mameneja wa Premier League katika msimu ujao kama mchezaji huru.'    


''Ufaransa wanamuhitaji yeye, kama ambavyo wanamuhitaji Zlatan Ibrahimovic. Ni mzuri kwenye Ligi lakini bila shaka atarejea Premier League.''     

''Ni kitu gani meneja halisi atakifanya? Kumchezea kamali mshambuliaji kwa euro millioni 100 au kumchuka Balotelli? kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuniambia kuwa sio mchezaji mwenye kipaji duniani.   



 
 

No comments:

Post a Comment