Saturday, September 17, 2016

KLOPP AENDELEA KUVUNJA DARAJA AIPIGA CHELSEA 2-1 STAMFORD BRIDGE'S.

                                            Klopp akifurahia ushindi na Henderson aliefunga goli la pili.

Jurgen Klopp ameweza kuendeleza rekodi yake ya kuifunga Chelsea katika uwanja wa nyumbani kwao ''Stamford Bridge's'' baada ya hapo jana kuwafunga 2-1 kwenye mchezo wa Premier League. magoli ya Dejan Lovren dakika 17 na Jordan Henderson dakika 36 yalitosha kuendeleza rekodi ya timu hiyo kuvunja mwiko wa kutoifunga Chelsea nyumbani kwao.   


                     Lovren akipongezwa na wachezaji wenzake mara baada ya kufunga bao.

Huo unakuwa ushindi wa pili wa Klopp dhidi ya timu hiyo ambapo hata msimu uliopita baada ya kuichukua timu hiyo aliweza kuifunga Chelsea Stamford Bridge akiwa katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu toka awe kocha wa Liverpool.    


                               Costa akipongezwa na wachezaji wenzake wa Chelsea.

Huku mchezaji matata wa Chelsea Diego Costa akisawazisha dakika ya 61 goli ambalo halikuweza kuwatoa kimasomaso nyumbani kwao.

Ilikuwa ni mechi ambayo ilisubiriwa na wengi kutokana na historia iliyokuwepo hapo mwanzo ya Liver kushindwa kuondoka na ushindi Stamford Bridge, lakini toka Klopp aichukue timu hiyo anaendelea kuvunja mwiko huo na kuwafunga Chelsea Stamford Bridge.   




No comments:

Post a Comment