Friday, September 16, 2016

KAKA WA MESSI APEWA ADHABU YA KUWA KOCHA KAMA SEHEMU YA HUKUMU YAKE



Lile jinamizi la kesi juu ya familia ya nyota wa Barcelona kuonekana kuendelea baada ya kaka wa mshambuliaji huyo kukutwa na hatia katika kesi mpya ya sheria dhidi ya Matias Messi na kulazimishwa kuwa kocha wa mpira wa miguu kama aina ya huduma za jamii kutokana na kesi yake ya kumiliki bastola kinyume na sheria mwaka uliopita.       

Matias anatakiwa kutumia masaa 4 kwa wiki katika kuziongoza na kuzifundisha timu za mitaani kwa mwaka mzima katika mitaa ya Rosalio, kwa mujibu wa hukumu ya Jaji Gonzalo Lopez Quintana. 

Matias pia anatakiwa kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya na pombe, na kutakiwa kulipa peso 8,000 kama faini.  

Lionel Messi na baba yake Jorge walihusishwa kwenye kesi ya kukwepa kodi, ambapo walikutwa na hatia mapema katika msimu huu mwezi wa July.   
 

 

No comments:

Post a Comment