Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Andres Iniesta ameweka bayana kuwa hafahamu juu ya hatma yake kama klabu hiyo itamruhusu kuweza kustaafu soka lake akiwa Nou Camp.
Iniesta ambaye ana mkataba na miamba hiyo ya Catalunya mpaka June 2018 ana nia ya kutaka kusaini mkataba mpya lengo lake likiwa kuendelea kubaki Barcelona mpaka wakati atakapomaliza soka lake na kustaafu.
Na Barcelona bado hawajaonyesha nia ya mazungumzo na Iniesta, ingawa amekubali kuwa suala hilo liko nj'e ya uwezo wake kama atatundika buti na Mabingwa hao wa Hispania.
''Ningependa kumalizia kazi yangu nikiwa Barcelona .'' Iniesta mwenye umri wa miaka 32 aliiambia Cadena COPE.
''Nina mkatba mpaka 2018. Itatubidi kuuliza mwelekeo kama watataka kupanua mkataba wangu.
''Lakini kitu pekee ninachoweza kurudia kuwa ninaitaji kustaafu nikiwa Barcelona.''
Iniesta ambaye alitokea kwenye safu ya kituo cha vijana cha Barcelona na mpaka sasa ameshacheza mechi 600 kwenye mashindano yote ya Barca toka alipojiunga nao mwaka 2002-03.
Na ameshashinda mara nane Kombe la LaLiga kipindi alichokuwa Nou Camp, na Champions League mara nne.
No comments:
Post a Comment