Thursday, September 22, 2016

ALIKO DANGOTE BADO ANA NIA YA KUINUNUA THE GUNNERS.


Tajiri namba moja wa Afrika anayetokea nchini Nigeria Aliko Dangote kwa muda mrefu amekuwa na nia ya kutaka kumiliki klabu ya Asenal lakini sasa ameweka wazi nia yake ya kutaka kuimiliki klabu hiyo ya washika bunduki wa jijini London Arsenal ndani ya miaka minne mbele.


Dangote ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa $ 10.9 billion pia alieleza juu ya dhamira yake ya manunuzi ya timu hiyo inayoshiriki Premier League mwaka jana.  Amesema kuwa anahitaji kusubili matarajio yake katika biashara zake kuboresheka na uwekezaji wake katika bomba la gesi na kusafishia mafuta kabla ya kufanya upatikanaji.  

''Hakuna shaka nitainunua Arsenal na hakuna tatizo la juu ya pesa,'' Dangote alisema kwenye mahojiano yake na Bloomberg Televion New York Jumatano hii.  

Dangote alisema ''labda kwa miaka tatu au minne. Suala ni kwamba tuna changamoto zaidi kwenye njia yetu upepo-kichwani. Naitaji kuziondoa kwanza katika njia alafu ndio nitaanza kuwa na upepo mkiani.''    

Dangote ambaye ni shabiki wa Arsenal, amepoteza $4.4 billion mwaka huu baada ya anguko la thamani ya fedha ya Nigeria.
Wingi wa utajiri wake uko jijini Lagos Nigeria ambako ndiko makao makuu yake ya Dangote Cement Plc yalipo.       

Dangote alisema, ''sio kuhusu kuinunua Arsenal na kuendelea na biashara kama kawaida.  

''Bali ni kuhusu kuinunua Arsenal na kuigeuza. Ninaendesha biashara zilizofanikiwa na ninazani kuwa naweza kuendesha timu yenye mafanikio.''   

''Kwasasa tunakabiliana na miradi zaidi ya $ 20 billion, siwezi kuvifanya vyote kwa pamoja.''  

Kama atafanikiwa kuimiliki Arsenal kutamfanya kuwa mmiliki wa kwanza kutoka Afrika kuwa na timu Premier League.  
 

No comments:

Post a Comment