Wednesday, September 14, 2016
JERAHA LA MGUU LAMUWEKA TERRY NJE KWA SIKU 10 AU ZAIDI
Nahodha wa Chelsea John Terry atakuwa nj'e ya uwanja kwa siku kumi au zaidi, baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi waliyotoka sare ya 2-2 na Swansea City.
Kcha wa Chelsea Antonio Conte alithibitisha baadaa ya mchezo huo (Jumatatu) kuwa mchezaji huyo aliumia na wanasubili repoti ya madaktari.
Na kupitia tovuti ya Chelsea walitangaza kuwa Terry anahitaji siku kumi au zaidi kurejea uwanjani, hivyo kutamfanya kukosa michezo miwili kati Liverpool siku ya Ijumaa wiki hii na Jumanne ijayo Kombe la Ligi dhidi ya Leicester City.
Kukosekana kwa Terry kutampa nafasi David Silva kufanya kazi yake kwa mara ya pili toka arudi Stamford Bridge siku ya mwisho ya usajili, huku kijana mpya Marcos Alonso kuwa chaguo lingine kwenye kuingia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment