Wednesday, September 14, 2016

MADRID TULICHUKIWA KIPINDI CHA MOURINHO -PEPE



 Beki wa Real Madrid Pepe anaamini kwamba timu hiyo ilikuwa ikichukiwa kipindi ambacho ilikuwa chini ya Jose Mourinho na beki huyo ameelezea furaha yake baada ya kocha huyo kuondoka.   

Mourinho alijiunga na Madrid 201 baada ya kupata mafaniko akiwa na Inter Milan ya Italia, akaweza kushinda La Liga 2011-2012 huku akikosa kombe la Champions League.  

''Chini ya Mourinho watu walituchukia tulipotoka nj'e ya uwanja.'' alisema Mbrazil huyo mwenye utaifa la Ureno aliiambia Cadena Ser.    

''Imepita miaka mitatu na ninamshukuru Mungu imepita haraka''   

''Mambo yalibadirika pale alipokuja Ancelotti, kwani uliona jinsi watu walivyobadirika na kuanza kutuchukulia tofauti''. Pepe ambae alipitia uhusiano mgumu na Mourinho, lakini sasa anafurahia maisha tena akiwa chini ya Zinedine Zidane  aliemrithi Rafael Benitez January.   

''Kilichotokea kwa Mourinho kimeshapita sasa niko imara na nimeshaachana nayo sasa hivi naimarisha nafasi yangu kuwa ngazi ya juu Real Madrid,'' aliongezea beki huyo.    

''Mourinho na Zidane ni watu wawili tofauti, mmoja unaweza kusema kuwa yuko kinyume lakini sio kwamba mmoja ni mbaya na mwingine ni mzuri.''    

''Mourinho ni mzuri mwenye ujuzi na uzoefu mwingi kama kocha, akiwa na timu kubwa na wacjezaji wazuri na imara. Zidane ndio kwanza ameanza La Liga mwaka uliopita lakini alicheza katika ngazi kubwa na anajua kinachotakiwa uwanjani.'' 



''Zidane alikuwa mchezaji na anajua tunachofikiria, sababu alikuwa na kazi nzuri akiwa Real Madrid, hivyo anaelewa shinikizo linavyokuwa.'' 

Beki alisema kuwa wanahitaji kujaribu bahati hiyo sababu itakuja kufika mwisho siku yoyote, kwani kocha wao huyo amewapa nafasi ya kujiamini kwa kutokusajili mchezaji mpya.  

Madrid ambao walifunga Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati kwenye fainali  msimu uliopita wa Champions League, wataendelea na kampeni yao ya kutetea taji lao Jumatano hii nyumbani kwao dhidi ya Sporting CP kwenye kundi F.   

No comments:

Post a Comment