Friday, September 16, 2016

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII, AZAM NA SIMBA UWANJA KITENDAWILI.


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hapo kesho Septemba 17, 2016. Kwa michezo sita katika viwanja tofauti na Mikoa tofauti. Ratiba ni kama ifuatayo hapo chini;

 
Azzam - Simba

      17.09.2016 14:00

Majimaji - Ndanda      17.09.2016 14:00

Mbeya City - Tanzania Prisons      17.09.2016 14:00

Mtibwa Sugar - Kagera Sugar      17.09.2016 14:00

Mwadui - Young Africans      17.09.2016 14:00

Ruvu Shooting - Mbao      17.09.2016 14:00



Lakini wengi wakiutazama mchezo baina ya Azam FC na Simba SC ambao wanavutana juu ya uwanja wa kuchezea timu hizo, hii ni baada ya TFF kuutoa mchezo huo katika Uwanja Wa Taifa na kuupeleka Uwanja Wa Uhuru ''Shamba la bibi''  kupisha mazoezi kwa timu ya Taifa ya Congo-Brazzaville chini ya miaka 17 ambao watacheza na Serengeti Boys Septemba 18 kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17. Huku TFF wakisisitiza kuwa hali ya usalama Chamazi hairidhishi ndio maana wamepeleka mchezo huo uwanja wa Uhuru. 
 

Azam ambao ratiba inaonyesha kuwa ndo wenyeji wa mchezo huo wanataka wakacheze kwenye uwanja wao wa Azam Complex uliopo chamazi na si kwingine, na kama watapeleka timu Uwanja wa uhuru basi ifahamike kuwa Simba ndio atakuwa mwenyeji wa mchezo huo na mchezo wa marudiano ukafanyike Chamazi kwenye uwanja wao kama wenyeji.    

Pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali sababu toka Azam waingie kucheza Ligi Kuu wamekuwa ni chachu ya upinzani kwa timu za Simba na Yanga  ambazo zilikuwa zikipishana ubingwa wa Ligi kuu na kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye michuano ya Kimataifa lakini uwepo wake umekuwa na upinzani juu ya kuwania nafasi za kufuzu kucheza michezo ya kimatifa kwa Simba ambao kwa misimu miwili hawajaweza kucheza michuano yoyote ya kimataifa huku Azam akifuzu kama mshindi wa kwanza au wapili wa ligi.  

Mchezo huo ambao una sintonfahamu ulipelekea Msemaji wa Simba SC Haji Manara kusema kuwa hata kama Azam watataka wakacheze kwenye viwanda vyao vya Bakhresa wako tayari kwani  dakika 90 ndio muamuzi, huku akiunga mkono kwa Azam kutaka kucheza kwenye uwanja wake wa Chamazi kwa mechi za nyumbani lakini Manara alisema kuwa tahadhari ya usalama inayotajwa kwamba ni tatizo Chamazi inapaswa kuzingatiwa.   

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotoka mwezi wa July, mchezo wa Azam na Simba unapaswa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa huku Azam wakiwa wenyeji wa Simba.  

 

No comments:

Post a Comment