Saturday, September 17, 2016
NDOTO YANGU SIKU MOJA KUICHEZEA MAN UNITED- KESSIE
Kessie raia wa Ivory Coast anaechezea Atalanta baada ya kukosa kibali cha kazi nchini Uingereza ambaye alikaribia kujiunga na Sunderland kwenye kipindi cha usajili.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye ana mabao 4 katika mechi 5 alizocheza kwenye mashindano yote akiwa na tiimu hiyo ana matumaini ya kuichezea Manchester United siku moja kwa siku za mbeleni.
''Nina wachezaji wawili ambao nawapenda Yaya Toure na Michael Essien. Najifunza mengi kutoka kwao,'' aliiambia Sky Italia.
''Essien anakimbia sana na Toure anashambulia sana. Wameniambia nifanye kazi kwa bidii kufikia kiwango chao.''
''Naipenda Premier League, lakini kwa sasa hapana, nahitaji kujifunza mbinu za Italia, na labda siku moja naweza kwenda Man United.'' Sielewi kama Mourinho bado atakuwepo, lakini ni timu ambayo siku zote naipenda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment