Tuesday, September 13, 2016
KUTOKUWEPO KWA IBRAHIMOVIC HAIATHIRI PSG -BELLERIN
Wakati leo ikishuka dimbani kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG, mchezaji wa Arsenal Hector Bellerin anaamini kuwa kutokuwepo kwa Ibrahimovic kwenye timu hiyo ambaye amejiunga na Manchester United akutaiathiri timu hiyo kwenye mechi ya leo kwenye uwanja wa Parc des Princes, Paris Ufaransa.
The Gunners ambao wanaanza kampeni yao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG leo Jummanne kwenye hatua ya makundi, ingawa Mabingwa hao wa Ligue 1 hawakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi yao ya Ijumaa dhidi ya Saint Etienne.
Lakini pamoja na matokeo hayo, Bellerin anaamini hakutowafanya wapinzani wao kufanya mashambulizi bila Ibrahimovic, ambaye alifunga magoli 50 katika mechi 51 alizocheza msimu uliopita na timu hiyo.
Ibrahimovic aliefunga goli 50 katika mechi 51 na PSG msimu uliopita.
''Kama klabu ina wachezaji wengi wazuri hivyo kukosekana kwake Ibrahimovic sidhani kama kutawaathiri(PSG).'' alisema Bellerin
''Tayali wana wachezaji wenye nguvu watatu na mchezaji yoyote atakaepanda mbele itakuwa ni hatari kwetu''
''Inatubidi tukabiliane na mechi kama vile ambavyo Ibra alikuwa akicheza'' tunajisikia kufanya hivyo.
Pia alimzungumzia Di Maria na kusema kuwa ''ni mchezaji mzuri na mwenye kutumia mguu wa kushoto na itakuwa ni vigumu kumzuia'', alisema Mhispania huyo.
''Lakini tumeshakabiliana na wachezaji wenye ubora kabla yake na hivyo tuko tayali kumkabili na yeye pia.''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment