Tuesday, September 13, 2016

KWANGU NYOTA WA BARCELONA LUIS SUAREZ NDIE MCHEZAJI BORA DUNIANI -RODGERS


Kocha wa timu ya Celtic ya Scotland ambao leo wanashuka dimbani Nou Camp dhidi ya Barcelona kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambaye aliwahi kumfundisha nyota wa Barca Luis Suarez kipindi wakiwa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa anaamini stireka huyo ndiye mchezaji bora duniani.   

Brendan Rodgers anaamini kuwa vijana wake watapaki mabasi mawili Nou Camp ili kuweza kuwazuia nyota wa Barcelona, aliwaambia Press Association Sport.  

Stireka huyo mwenye umri wa miaka 29  aliwahi kufanya kazi na Rodgers Liverpool atashirikiana na wachezaji wenzie Lionel Messi na Neymar kuwakabili vijana wa Rodgers wanaojulikaana kama 'Hoops'.   

Rodgers ambae amesisitiza kuwa Luis Suarez ni mchezaji bora alisema kuwa ''kwanza ukianza kumzungumzia Suarez unakuwa unamuongelea mwanaume'', kwanza ni mmoja wa wanaume wazuri ambao hela umfata''. Na sidhani kama kuna maswali juu ya hilo. 

                     Suarez walipokuwa na Rodgers Liverpool.

''Ni kijana mnyenyekevu, anaefanya kazi bila kuchoka katika taaluma yake. Yeye ni mtaalamu kitaaluma, ni mtu wa familia ambaye huwapa kila kitu kwa maisha yake kama mchezaji na maisha yake.''  

''Nilipata bahati ya kufanya nae kazi kwa miaka miwili na alikuwa wa ajabu kama mchezaji, yeye ni bora duniani.'' Pongezi kubwa naweza kutoa kwa Luis ambaye yuko kwenye timu kubwa duniani na tayali ameshawafanya kuwa bora.  

                     Celtic watakabiliana na Barcelona-MSN.

''Na kila nikiwaona wakicheza  sasa, Barcelona haiwezi kuwa sawa kitimu bila Suarez.'' Huku kocha huyo akisisitiza kupaki basi kwenye mchezo huo wa leo, ambao anaamini utakuwa mgumu kwa upande wao. 
 


 

 

No comments:

Post a Comment