Saturday, September 3, 2016
MASCHERANO AMWAMBIA DYBALA KUKUMBUKA KADI NYEKUNDU YA MESSI 2005
Mchezaji mkongwe wa timu ya taifa ya Argentina Javier Mascherano, amemwambia mchezaji mwenzake Paulo Dybala kukumbuka kadi nyekundu aliyowahi kupewa Messi dhidi ya Hungary mwaka 2005 kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 18 tu. Dybala, alitolewa nj'e kabla ya mapumziko kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia alhamis iliyopita dhidi ya Uruguay waliyotoka kifua mbele kwa 1-0 bao lililowekwa wavuni na Messi. Mascherano amesema amejaribu kutumia mfano huo kumuweka sawa Dybala ''nilimwambia kitu kama hicho kiliwahi kumtokea Messi pale alipoanza kuchezea timu ya taifa''.Messi alifungua kalamu yake ya magoli kwa taifa lake toka amerejea kikosini baada ya kutangaza kuachana na timu ya taifa mwezi wa sita mwaka huu baada ya kupoteza fainali ya Copa America dhidi ya Chile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment