Saturday, September 3, 2016
MOYO WA ALCACE'R ULIKUWA BARCA 'RAIS WA VALENCIA'
Rais wa timu ya Valencia Chan Lay Hoon anaamini mchezaji Paco Alcace'r moyo wake ulikuwa kwa mabigwa wa la liga Barcelona kabla ya uhamisho wake kwa mabingwa hao. Alcace'r 23, amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona jumanne iliyopita akiachana na timu yake ya utotoni kwenye uhamisho uliogharimu euro 30 milion. Bi Chan alihuzunishwa na maamuzi ya Alcace'r kuondoka Mestalla lakini amesema Valencia walikuwa na maamuzi kidogo juu ya kuondoka kwake lakini ilibidi wamruhusu ''alikuwa ni shujaa na alama kwetu na alikuwa nasi toka akiwa na umri wa miaka 11''
''lakini kama mtu ni shujaa na moyo wake uko sehemu nyingine haingii akilini kuendelea kuwa nae'', bi Chan alisema klabu ilikuwa inataka kumbakisha Alcace'r aliesahini miaka mitano na Barca. Ilikuwa ni maamuzi magumu ya klabu kutomruhusu kuodoka naelewa ni ngumu kwa mchezaji kuikataa Barca inapomuhitaji.
Alcace'r aliifungia magoli 13 Valencia msimu uliopita na 11 msimu wa 2014-2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment