![]() |
Lionel Messi akitoka hapo jana baada ya maumivu ya misuli. |
Bingwa huyo mara tano wa Ballon d'Or alitolewa kipindi cha pili cha mchezo kabla ya wageni kusawazisha bao.
Ofisa wa Barcelona alithibitisha kukaa nj'e kwa nyota wao huyo, ''Leonel Messi amepata maumivu ya kinena upande wa mguu wake wa kulia na hivyo atakaa nj'e kwa wiki tatu.''
Mfungaji huyo wa muda wote Barcelona atakosa mechi za Ligi mbili dhidi ya Sporting Gijon na Celta Vigo na mchezo wa kundi katika Champions League dhidi ya Borussia Moenchengladbach.
Nahodha huyo wa Argentina pia atalazimika kuwa nj'e kwenye timu ya Taifa katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia, dhidi ya Paraguay na Peru.
Kama Messi atapona kwa wakati uliokusudiwa basi atarudi uwanjani katika mechi ya Barcelona dhidi ya Deportivo La Coruna Oktoba 15.
''Mimi sio daktari na siwezi kusema lolote lakini Messi akiumia wote tunapoteza, soka linapoteza,'' kocha wa Barcelona Luis Enrique alisema hayo.
Messi ambae alilazimika kukosa mechi nane msimu ukiopita baada ya kuumia goti lake, lakini Barca walishinda mechi nane katika kumi bila ya nyota wao huyo, na Luis Enrique amesema kuwa hana shaka na timu yake itakavyokuwa bila ya Messi.
''Msimu uliopita tulikuwa katika hali kama hii lakini timu ilicheza kwa kiwango kikubwa,'' alisema kocha huyo.
''Bila Messi tunakuwa tunapoteza uimara wetu kidogo lakini bado tutakuwa imara, natumaini atapona haraka na sisi tutaendelea kama ambavyo tunaendelea, kucheza kwa kujiamini.''
No comments:
Post a Comment