Thursday, September 22, 2016
MESSI AUMIA BARCELONA IKIPATA SARE NA ATLETICO MADRID NOU CAMP
Timu ya Barcelona hawakuweza kuzuia mambo mawili waliyopata katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid, baada ya Lionel Messi kutolewa nj'e ya mchezo baada ya kupata majeraha na pia kuzuia sare waliyoipata kutoka kwa wageni hao ya 1-1.
Ivan Rakitic ndie aliefunga bao la Barca ndani ya kipindi cha kwanza dakika ya 41 ya mchezo huo, kabla ya Angel Correa kusawazisha bao hilo dakika ya 62 za mchezo huo kipindi cha pili.
Huku nyota wao Lionel Messi akitolewa nj'e ndani ya kipindi cha pili baada ya kupata maumivu ya misuli kwenye kinena ambayo huenda yakamuweka nj'e kwa wiki kadhaa.
Neymar na Suarez walijitihidi kubadirisha matokeo lakini hawakuweza kutokana na upinzani walioupata kutoka kwa mabeki wa Atletico. Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa pande zote kutokana na kila pande kuimarisha safu yake ya ulinzi na kiungo.
Barcelona watashuka dimbani Jumamosi hii dhidi ya Sporting Gijon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment