Monday, September 12, 2016
RONALDO NAHODHA MPYA MADRID, GUARDIOLA ASEMA HAMNA BORA ZAIDI YA MESSI
Hakuna ubishi kuwa Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri na anaecheza mpira mzuri kwenye timu yake, kwa kutambua hilo Real Madrid wamempa unahodha wa timu hiyo.
Baada ya Alvaro Arbeloa kujiunga na West Ham na kufanya Los Blancos kutaka nahodha mpya na uteuzi huo unamfanya kuungana na manahodha waliopita katika kikosi chao hicho ambao ni Sergio Ramos, Pepe na Marcelo ambao walipitia majukumu hayo wakiwa pamoja.
Ronaldo alijiunga na Madrid 2009 na mpaka sasa ana misimu nane na Real Madrid, Mchezaji huyo amepewa heshima ya kuiongoza klabu hiyo kutokana na ubora wake na mafanikio anayoipa klabu hiyo.
Ilie vuta nikuvute ya nani bora kati ya Messi na Ronaldo kocha wa Manchester City Pep Guardiola ambaye pia aliwahi kuifundisha Barcelona amesema kuwa hakuna mchezaji bora zaidi ya Lionel Messi.
Alisema kuwa ''mchezaji bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ni Messi na hakuna bora zaidi yake.''
Kufunga magoli muhimu kadhaa kwa Barcelona kuelekea kwenye makombe mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Guardiola, Messi aliecheza mpira mzuri wakati wa Guardiola ambao unamfanya kukumbuka ushindi wote.
''Ilikuwa ni furaha kuifundisha Barcelona na Bayern Munich na kuzifikisha mbali katika Ligi ya Mabingwa Ulaya''' alisema kiungo huyo wa zamani, ''lakini sasa hapa Manchester City tuna historia yetu nyingine,''.
''Mimi sio mpenzi, ninataka kushinda michezo yote na ninadhani njia bora ya kushinda ni mali yangu, kitu ambacho ninajaribu kuwashawishi wachezaji wangu .''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment