Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Ufukweni, John Mwansasu amemuita kipa wa Mbeya City ya Mbeya Juma Kaseja Juma kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kinachotarajia kusafiri kwenda Abidjan kucheza na wapinzani wao Ivory Coast kwenye mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Kaseja mwenyewe, amefurahia wito huo wakati wowote anatarajia kujiunga na kambi hiyo iliyopo hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), uwanja wa Kumbukumbu wa Karume, Ilala jijini Dar es salaam.
Mwansasu amesema amesema kwamba Kaseja anaweza kumsaidia kwenye kikosi chake kwa kuwa mbiu za mchezo huo, nafasi ya kipa inaweza kuamua matokeo kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza timu ya mafanikio hivyo amemuita kwenda kusaidiana na Ahamed Rajab.
Nyota wengine wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahamd, Mohammed Makame, Ahamed Rajab(golikipa), Khamis Said,Yacob Mohamed, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kelvin Baraka.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka Septemba 14, mwaka huu kwenda Abidjan, Ivory coast ambako timu hizo zinacheza mchezo huo wa mwisho huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwenye fainali.
Itakumbukwa kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Agosti 26, 2016, hapa Dar es salaam, Tanzania ililala kwa mabao 7-3 katika mchezo uliochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao na Shafic Mugerwa aliyepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige na Muhammad Ssenteza wakati mtunza muda alikuwa Adil Ouchker wa Morocco na kamishna akiwa Reverien Ndikuryo wa Burundi.

No comments:
Post a Comment