Friday, October 14, 2016

CHIDIEBERE NJE WIKI SITA

agrey-chidiebere
Agrey Morris na Azam walipomtembelea Chidiebere.


Mshambuliaji wa Stand United raia wa Nigeria Abasirim Chidiebere atakuwa nje kwa wiki sita akiuguza majeraha yake ya kuvunjika taya aliyopata kwenye majukumu yake ya kikazi kwenye mechi ya Stand dhidi ya Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mshambuliaji huyo wa Stand alikutana na kadhia hiyo kutoka kwa beki wa Azam FC Agrey Morris kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa Stand kushinda 1-0 dhidi ya Azam ya jijini Dar es Salaam.

Huku taarifa ya daktari wa klabu hiyo akithibitisha kwamba mchezaji huyo atoweza kufungua  kinywa chake kwa muda wa wiki mbili kutokana na nyaya alizowekewa kwenye kichwa chake.   

“Kilichotokea, mchezaji wa Azam Agrey Morris alimchezea rafu mchezaji wetu Abasirim Chidiebere alimpiga taya, tuligundua muda huohuo kilichotokea kwamba aliumia sana tukampatia huduma ya kwanza hapohapo alikuwa anatokwa damu mdomoni tukamsaidia na badae akakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa lililokuwepo uwanjani,” amesema Dr. Peneheli .
“Alipofika hospitali wakagundua kwamba amevunjika taya wakamtafuta daktari wa meno na kinywa akaona amevunjika taya la chini upande wa kushoto na kulia, zaidi ameumia upande wa kushoto kwahiyo muda huohuo akapatiwa huduma, wamemfunga waya juu ya meno na chini ya meno kwa nyaya za kitabibu. 

Zinafungwa kiasi kwamba hawezi kufungua mdomo ili kuruhusu mpasuko huo upone.”
“Kawaida tunategemea mpasuko huo utapona kwa wiki sita, wakati huohuo alikuwa ametoka meno mawili, kwahiyo hapo mdomoni kuna njia ambayo itamuwezesha kulishwa vyakula laini kama supu ya dagaa, supu ya samaki ambazo zinakuwa na calcium nyingi, atapata juice ya asili na uji wa mtama au uwele ambao utaweza kupita kwenye mrija.”

“Anaendelea vizuri baada ya wiki mbili au tatu anaweza akaondolewa hizo nyaya lakini kwa kupitia kwa daktari wa kinywa na meno baada ya kuona inafaa. Tunategemea wiki sita hadi saba mpasuko utakuwa umeweza kupona.”

No comments:

Post a Comment