Sunday, October 9, 2016

EURO 2016 KWA MULLER NI NGUMU KUIELEZEA-LOW



Thomas Muller akishangilia moja ya mabao yake dhidi ya Czech.
Kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low amesema kwamba  Thomas Muller alikuwa na kiwango kibovu kwenye  michuano ya Euro 2016 kiasi ni ngumu kukielezea lakini akisema  ni kawaida kwa mshambuliaji.
Muller ambaye alishindwa kufunga bao lolote ndani ya dakika 570 za Euro na Ujerumani kufungwa na wenyeji Ufaransa kwenye nusu fainali. 


Lakini nyota huyo wa Bayern Munich ameanza cheche zake za ufungaji kwenye kuwania kufuzu Kombe la Dunia akishinda mara nne pamoja na mara mbili kwenye  mechi yao dhidi ya Czech Republic siku ya Jumamosi.    

Low ambaye anapata tabu kuelezea matatizo ya Muller kwenye Euro 2016, lakini anasema kwamba kila mshambuliaji ana kiraka chake.

''Siwezi kufikiria lakini tunapaswa kuangalia sababu maalum,'' alisema kocha huyo.    

''Kila mshambuliaji ana awamu yake, ambapo yeye hawezi kufunga mabao inakuwa bahati mbaya. Na hilo ndilo lilikuwa tatizo la Muller kwenye Euro.   

''Lakini ni mchezaji ambaye, siku zote anafunga mabao na ameonyesha hilo. Ni vigumu kulielezea. 

''Toka Kombe la Dunia 201, Thomas Muller amekuwa akifunga kwenye Bundesliga na timu yake ya taifa kwa kiwango kikubwa. Ni kawaida kuwa kwenye wakati mgumu kama ambao aliupitia kwenye Euro.''    

Muller ambaye pia alisema siku zote anajaribu kuwa mfungaji tofaiti na hali iliyotokea Ufaransa, na tayali ameshaiongoza Ujerumani kwenye ushindi miwili kwenye mechi za kufuzu.  

Alisema ''Siku zote ninasema kuwa siyapi kipaumbele kwa yale yanayosemwa. Sio kwenye ukweli au uongo.  

''Siku zote ninajaribu kukaa sehemu sahihi, na kuwasikiliza makocha wangu pekee na sauti ya ndani yangu. Kama kutakuwa kuna ushauri mzuri kutoka kwa waandishi wa habari, nitausikiliza pia.    

''Ninajaribu kuchukua mazuri na kuyatumia kwa kukaa kwa umakini. Kama mshambuliaji siku zote unapaswa kujaribu kubadili nafasi yako, na kutoa kila kitu kwenye mafunzo, ndio hivyo. 

No comments:

Post a Comment