Sunday, October 9, 2016

ROSBERG ASHINDA JAPAN GRAND PIX

Nico Rosberg akishangilia ushindi wake.
Nico Rosberg ameweza kushinda taji la Japan Grand Pix hapo jana nchini Japan na kumfanya kumpita bingwa wa dunia Lewis Hamilton kwenye mbio za ubingwa za Formula One ambaye alikuwa na mwanzo mbaya kwenye mashindano hayo.
Mjerumani huyo alisema kwamba ushindi wake wa Suzuka ni wa kwanza dhidi ya Hamiliton mbaye ameshika nafasi ya tatu baada ya kuanza vibaya, Rosberg ambaye ameongoza dhidi ya mpinzani wake wa Mercedes kwa pointi 33 kwenye mashindano manne ya msimu huu.   

''Wooooooh alisikika Rosberg akipiga kelele mbele ya timu ya redio baada ya ushindi wake wa nne kati ya tano tangu majira ya  mapumziko na ushindi wake wa tisa kwa 2016.   

''Ahsanteni sana marafiki zangu, wikiendi ya ajabu kwangu juu ya ushindi huu, aliongeza baada ya yeye na Hamilton kulinda ushindi wao mara tatu mfululizo.   

''Ni pointi 33 lakini mimi silengi hilo. Bado kuna safari ndefu ya kwenda hivyo mimi ninaweka akili yangu chini.'' 
 

No comments:

Post a Comment