Thursday, October 13, 2016

KIBIRA ASISITIZA USHIRIKIANO.

Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Kibira.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli (CHANETA) Ana Kibira amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kuanzia ngazi za Wilaya kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo.


Mweneyekiti huyo alisema ili kufikia lengo la kupata vipaji vipya, ni lazima kuwe na ushirikiano kuanzia wilaya na mkoa katika kuandaa mashindano yatakayosaidia kuwaleta pamoja.

Alisema lengo la kusisitiza ushirikiano mikoani haimaanishi kuwa hakuna ila si kiasi cha kutosha hivyo kuwataka wadau na viongozi wa mchezo huo kuuendeleza kwa manufaa ya wote.
“Tumekuwa na utaratibu wa kufanya mashindano ya netiboli kila mkoa, unajua peke yetu bila kuungwa mkono na wenyeji kama wilaya na hata mikoa hatutaweza, lakini tukiunganisha nguvu tutafanikiwa,” alisema.
Kibira alisema kwa ushirikiano ni rahisi kupata vipaji vingi mikoani ambavyo vitaibuliwa na kushirikishwa kwenye timu ya taifa.
Mwenyekiti huyo alisema mchezo huo umepoteza umaarufu siku za karibuni kwa kuwa, kulikosekana umoja na mshikamano kwa viongozi wa ngazi zote.
Chama hicho kinatarajia kufanya mashindano ya Ligi Daraja la pili yatakayofanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa mwezi huu.
Alihimiza timu kuendelea kuthibitisha ushiriki wao kwa ajili ya kupanga ratiba ya maandalizi.

No comments:

Post a Comment