![]() |
LeBron James na Dwyane Wade walipokuwa Miami Heat. |
Wade ambaye aliwahi kucheza timu moja na LeBron Miami Heat, alikuwa mchezaji huru msimu ulioisha kabla ya kujiunga na timu ya nyumbani kwao ya Chicago Bulls.
James ambaye aliamini Cavs wangemchukua Wade, lakini anaamini kuwa kuna sababu iliyopelekea kutofanikiwa kwa jambo hilo.
''Tusingeweza kummudu Wade,'' James aliwaambia ESPN.
Wade mwenye umri wa miaka 34, amesaini mkataba wenye thamani ya $ million47 kwa miaka miwili, mkataba ambao kwenye NBA una soko kubwa.
Wade ambaye bingwa mara 3 wa ubingwa wa NBA na mara 12 wa All-Star alikuwa na wastani wa pointi 19 kwenye kila mchezo wa msimu uliopita, lakini alipoteza hatua ya kusonga mbele.
huku kocha wa Cavs Tyronn Lue akikubali kwamba walikuwa wanamuhitaji Wade kwa sababu ya maendeleo yake mazuri, ila kama wangemchukua basi ilibidi wangemtoa mchezaji wao mmoja au kumuweka benchi ili Wade apate nafasi.
''Ndio tulimuhitaji Wade lakini kwa sasa haina jinsi.'' Alisema Tyronn Lue.
No comments:
Post a Comment