Thursday, October 6, 2016

KILA KOCHA ANAIFIKIRIA LIGI KUU YA UINGEREZA-BRADLEY


Bob Bradley kocha mpya wa Swansea ya Uingereza.



Baada ya kuwa kocha wa Swansea Bob Bradley amesema kwamba anafurahia kuwa kwenye ligi ambayo kila kocha katika dunia anaifikiria na kutaka kuijaribu. 

Mmarekani huyo ameajiriwa Oktoba 3 kuchukua nafasi ya Francesco Guidolin baada ya mwenendo mbovu wa timu hiyo ambapo ina pointi nne kutoka kwenye michezo yake saba ya kwanza ya ligi hiyo msimu huu, na kuwa eneo la kushushwa daraja juu ya tofauti ya mabao. 

Bradley ambaye amewahi kuzifundisha timu za taifa za Marekani na Misri pamoja na klabu ya Stabaek ya nchini Norway na klabu ya Le Havre katika Ligue 2. Na sasa ana msisimko wa nafasi aliyoipata kwenye ligi ya Uingereza. 

''Ligi Kuu ya Uingereza ni ligi ambayo kila kocha katika dunia anaiwaza na kutaka kuijaribu,''  Bradley aliiambia tovuti ya Swansea. ''Ukiangalia baadhi ya watu ambao wanafundisha kwenye Ligi Kuu kwa hivi sasa, na mimi kweli ninapata msisimko wa kufanya kazi katika ligi bora na kujaribu kuhakikisha tunafanya vizuri uwanjani, alisema. 

Bradley amejiunga na Swansea kipindi kigumu, ingawa anaweza kupata matokeo mazuri kwenye ratiba yake ngumu ya mechi zijazo ambapo zitakutana na Liverpool, Chelsea, Southamption, na kiongozi wa ligi hiyo Manchester City na bingwa mtetezi wa ligi hiyo Leicester City.   
 

No comments:

Post a Comment