Thursday, October 6, 2016

TITE AZUNGUMZIA UAMUZI WAKE WA KUMUANZISHA COUTINHO.

Image result for TITE,COUTINHO AND WILLIAN IMAGES



Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Tite amezungumzia uamuzi wake wa kumuanzisha Philipe Countinho mbele ya Willian kwenye mechi zao zinazokuja kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia.
  

Nyota huyo wa Liverpool anatarajiwa kuanza kabla ya Willian kwenye mechi dhidi yao na Bolivia na Venezuela.   

Willian ambaye alianza kwenye mechi mbili, huku Countinho akiwekwa benchi hali iliyoonyesha doa lake.  

Kocha huyo alisema mechi mbili na Countinho, ni wakati wake na ujuzi, si tu kwasababu mpinzani alikuwa amechoka.''  

Kwenye michezo yake miwili imeonyesha mafanikio, ushindi wa 3-0 dhidi ya Ecuador na ukifatiwa na ushindi 2-1 dhidi ya Colombia.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 amesema anataka kuona timu yake ikihimarisha viwango vyake.   

''Pointi tatu za Ecuador ni muhimu sana ni sawa na tatu za Argentina,'' alisema Tite ''lengo ni kufuzu.'' 

Brazil iko nafasi ya pili katika CONMEBOL katika kufuzu Kombe la Dunia, nyuma ya kiongozi Uruguay.

No comments:

Post a Comment