Monday, October 10, 2016

KUMUACHA ROONEY ITAKUWA VIZURI KWA SLOVENIA- KATANEC.

Image result for wayne rooney images in england team

Kuelekea mchezo wao dhidi ya England kwa ajili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, kocha wa timu ya taifa ya Slovenia Srecko Katanec amesema kwamba kuachwa kwa nahodha huyo kwenye mechi dhidi yao Jumanne hii litakuwa jambo bora.
 Timu hizo ambazo zitacheza Ljublijana Jumanne hii, huku kukiwa na taarifa kutoka kwa kocha wa England Gareth Southgate kuwa na mpango wa kumtema nyota huyo wa Manchester United kwenye kikosi chake hicho.

Wayne Rooney yuko kwenye wakati mgumu ambao anakabiliana na zomea zomea ya mashabiki ndani ya klabu yake na timu ya taifa, na hilo lilijidhihirisha Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa England dhidi ya Malta ambapo walishinda 2-0 kwenye Uwanja wa Wembley lakini mashabiki walimzomea mchezaji huyo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye mechi hiyo. Huku mwenye akisema ataachana na timu hiyo baada ya fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.

Licha ya yote hayo Rooney anashikilia rekodi ya ufungaji kwenye timu yake ya taifa ya England, huku akifunga goli moja kwenye mechi kumi na mbili alizocheza kwenye klabu na nchi yake kwa msimu huu, lakini Katanec anatarajia kumuona kwenye benchi la mabadiliko.

''Ningeshauri kama asingeanza, Katanec alisema hayo kwenye mahojiano na  chumba cha habari.'' Bado ni kiongozi kwa England.

''Lakini sitoshangaa kuona kama hatoanza mchezo huo. Sio mdogo na labda aina yake ya uchezaji imemzamisha kidogo.''

''Yeye ni kiongozi na kama kiongozi ni mtu aliyecheza mechi nyingi sana kwenye timu ya taifa, mtu kama huyo sio rahisi kumtoa nje.

''England ni timu bora kwenye aina zote na tunatarajia itakuwa ni mechi ngumu kwetu.''


England ambao wanaongoza kundi F wakiwa na pointi sawa kutoka kwenye mechi zao mbili, huku Slovenia wakiwa watatu na pointi nne.

No comments:

Post a Comment