Huenda mshambuliaji wa Bayern Levekursen Javier Hernandez ''Chicharito'' akarudi Real Madrid baada ya Mkurugenzi Santiago Aguado kusisitiza kurudi kwa nyota huyo, ambaye alitumia msimu wa 2014/2015 akiwa Madrid kwa mkopo akifunga mabao tisa katika mechi 33 kabla ya Man United kumuuza kwa Leverkusen.
Mkurugenzi huyo Santiago Aguado amependekeza kwamba milango iko wazi kwa mchezaji huyo kurudi Madrid, baada ya Mmexico huyo kufanya makubwa akiwa Leverkusen, ambapo kiungo huyo ameshafunga mabao 33 katika mechi zake 55 akiwa Bayern Leverkusen toka 2015 akitokea Manchester United.
Na pengine kiwango hicho kimemshawishi Mkurugenzi huyo aliiambia Fox Sports ''ndio ninapenda kumuona Chicharito akirudi Madrid tunadhani ni mchezaji bora.''

No comments:
Post a Comment