![]() |
| Jeneza lenye mwili wa Mike Towell. |
Mabondia na washabiki wa mchezo huo wameungana na familia ya marehemu Mike Towell kwenye safari yake ya mwisho hapa duniani leo hii kwenye kanisa la St Andrew Cathedral huko mjini Dundee.
Bondia huyo aliyekuwa na umri wa mika 25 alifariki dunia hospitalini Septemba 30 mwaka huu baada ya kupata majeraha kwenye pambano dhidi ya Dale Evans.
Evans pia alikuwa mmoja wa waliohudhuria mazishi hayo.
Marafiki wengi na wajumbe wa klabu yake ya ngumi walivalia mafulana meupe yenye picha yake yakiwa na ujumbe wa ''Mwamba towell'' huku wengine wakivaa masweta yaliyobeeba ujumbe uliosomeka ''Bingwa wa Dundee'', ''Shujaa ataishi milele'' au ''Team Towell.''
Huku familia ya marehemu Towell ikitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na kuwatia moyo kipindi chote hicho.
Familia hiyo ilisema ''leo ni siku ngumu kwetu na kila mmoja wetu, ni siku ambayo tunaamini kwamba Mike hatorudi nyumbani pamoja na sisi.
''Hata hivyo ni kipindi kila mmoja yuko na sisi kutufariji.''
Pia tunamshukuru Evans kwa uwepo wake na kuwa pamoja na sisi hapa kututia moyo kwani toka hospitali alikuwa pamija nasi, kwetu sisi tumempoteza mtoto, baba, rafiki, shujaa na mpenzi. Lakini tutaendelea kumkumba siku zote na kuendelea kutoa tabasamu kwenye kila ukumbusho wake.

No comments:
Post a Comment