Friday, October 14, 2016

ULAYA KUZUILIWA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2026.

Timu ya taifa ya Ujerumani kikishangilia ubingwa wa Kombe la Dunia 2014.
Nchi za ulaya hazitaweza kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2026 kutokana na sera za mzunguko wa Fifa.
 2026 mashindano yanaweza kuhusisha timu 40-48 baada ya baraza la Fifa kukubali kujifunza kwa undani zaidi jinsi ya kuchagua na kupanua mashindano kutoka kwenye mfumo wake wa timu 32. 

Mapendekezo hayo yatafanywa kwenye mkutano wa Fifa January 9, 2017.

''''Hisia zinazotolewa na wanachma wa baraza ni kwamba zinaunga mkono upanuzi'',alisema rais wa Fifa Gianni Infantino. 

Huku akiongezea kwamba ''vijana wadogo wanahitaji kucheza makampuni wanataka kujihusisha na udhamini zaidi sababu faida ya faida ya mpira wa miguu ni kubwa zaidi.  

Lakini ameshaanza kupingwa na wadau wa soka huku wakionyesha wasi wasi wao juu ya kudhohofisha ubora wa soka katika fainali hizo.   

kombe la Duina 2018 litafanyika nchini Russia na 2022 nchini Qatar.

No comments:

Post a Comment