Saturday, October 8, 2016

MIAKA KUMI BILA RAUL LALIGA, UTAFITI WAONYESHA NI MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA.

Ikiwa imepita miaka kumi bila uwepo wake kwenye LaLiga , utafiti wa nchini humo umeonyesha kwamba toka kuanzishwa kwa ligi hiyo mwaka 1928 Raul anaonekana mchezaji bora kuwahi kutokea.
Kituo cha Utafiti cha Hispania [CIHEFE] imetumia kanuni kuweka sawa na kuamua nani bora kwenye mpira wa kikapu, tenisi, baiskeli na wanariadha na kuwapa pointi kutokana na malengo yao na kukabiliana kwao kwenye majukumu yao ya kimichezo. 

Kwa hatua hii, pointi za wachezaji zilitolewa miongoni mwa wachezaji wengine, pointi 20 kuzingatia dakika alizocheza kwa msimu, pointi moja ya bao,  kupoteza mchezo na kadi nyekundu.

Jose Antonio Ortega ambaye ndie mkuu wa utafiti huo, aliyeandaa taarifa hii na kujiridhisha kwamba, akiwa na pointi 528 mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid Raul anabaki kuwa juu na kuwa mchezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya LaLiga. Kiungo wa zamani wa Barcelona Cesar Rodriguez aliewahi kushinda Mataji matano ya LaLiga ndani ya miaka 16 aliyokaa Nou Camp amepata pointi 524 na Telmo Zarra wa Athletic Club akipata 493.

Lionel Messi anakuwa mchezaji bora wa sasa kwa pointi 490 na kumweka Muargentina huyo kuwa nafasi ya nne ambaye maisha yake ya mpira akitumia akiwa Barcelona na kupata mataji nayo. 

Nafasi ya tano ilienda kwa Quini, aliyekuwa mshambuliaji maarufu wa muda mrefu wa Blaugrana na Sporting Gijon 1960-1980.

Utafiti huo ambao ulionekana kama vile una upendeleo na washambuliaji mfano mshambuliaji Artiz Aduriz amepata pointi 109. Lakini utafiti huo unaonyesha umuhimu wa kukaa kwa muda mrefu kwenye klabu moja kama njia ya kujenda urithi kwenye LaLiga.  

Huku Cristiano Ronaldo alishika nafasi ya 23, David Vila 32, Xavi 49, na Iker Casilas 62.  


 



No comments:

Post a Comment