![]() |
| Amir Khan akifanya mazoezi kwa ajili ya kurejea kwake. |
Baada ya kuumia mfupa wa mkono miaka 13 iliyopita bondia wa Uingereza Amir Khan anatarajiwa kurudi ulingoni mapema mwakani.
Bondia huyo ambaye amethibitisha kupona kwake kupitia akaunti yake ya instagram kwamba sasa yuko fiti baada ya upasuaji mara mbili aliofanyiwa.
''Upasuaji wa kwanza ulifanyika vizuri. Na wapili ukawa bora zaidi.''
Alisema bondia huyo huku akiweka picha zake za Xray kwenye akaunti yake hiyo.
''Niliteseka na maumivu ya mkono wangu wa kulia kwa miaka 10. Nilisubili na kupigana kwa njia hiyo kama tekinolojia ya kisasa zaidi nikaamua kuipata.
''Lakini sasa tayali mkono wangu unahisi ajabu, nataka kupiga mfuko ngumi lakini daktari anashauri kuendelea kushikilia na kusubili kwa muda wa wiki nne. Mkono wangu unawasha na ninataka kupiga ngumi kutumia mkono wangu mpya wa nguvu 100%.

No comments:
Post a Comment