Saturday, October 15, 2016

MOYES AFIKIRIA KIBARUA CHA TIMU YA TAIFA YA SCOTLAND.

David Moyes kocha wa Sunderland.
Kocha wa Sunderland David Moyes ameweka wazi nia yake ya kutaka kuifundisha timu ya taifa ya Scotland lakini akisistiza kuwa  Gordon Strachan anabaki kuwa kocha sahihi kwa taifa hilo.

Maisha ya Strachan kwenye timu hiyo ya taifa ya Scotland yako mashakani baada ya Scotland kukusanya pointi moja tu kwenye kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwenye mechi zake dhidi ya Lithuania na Slovakia.    

Scotland ambao walipata sare dhidi ya Lithuania lakini walipoteza kwa 3-0 dhidi ya Slovakia Jumanne iliyopita. Huku Moyes akiwa na shauku ya kulinoa taifa hilo lakini akisisitiza Strachan aendelee kulinoa taifa hilo, ingawa wana hali ngumu. 

''Kitu cha kwanza ninachoweza kusema ni kwaba Gordon anafanya lile awezalo kuweza kuisadia timu kwa alichonacho,'' alisema Moyes, 

''Ukizingatia, hilo ndilo ninalofikiria. Scotland ni nchi yangu na ninaiunga mkono  na kuifatilia toka nikiwa mdogo, lakini kwa kilichopo kwa Gordon ni vugumu kwa yeye  kufanya zaidi.  

''Anajitahidi kufanya yaliyo bora kwa timu, kwangu Gordon ni mtu sahihi kwa timu.    

''sitoweza kusema kwamba sitokuja kuifundisha Scotland kwa siku zijazo. Ni kitu ambacho kila siku ningependa kuwa wazi.''  



No comments:

Post a Comment