Tuesday, October 4, 2016

MWADUI FC WATHIBITISHA KUONDOKA KWA JULIO HAKUTAACHA PENGO KLABUNI HAPO.


Ikiwa imepita siku moja toka aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jamhuri Kihwelu kutangaza kuachana na kufundisha soka hapa nchini, kutokana na maamuzi ya waamuzi wa mchezo wa soka kutotenda haki juu ya maamuzi yao kwenye mechi za soka nchini.
Uongozi wa klabu ya Mwadui FC umesema kuwa kuondoka kwa kocha huyo hakutakuwa na pengo lolote kwani wapo makocha wengi wanaohitaji kuifundisha timu hiyo. 

Juzi Jumapili Jamhuri alitangaza kuachana na soka la nchini kufuatia timu yake kufungwa na Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom huku akionyesha kutokubaliana na maamuzi yatolewayo na waamuzi mbalimbali wa soka hasa katika kutotenda haki.   

Katibu Mkuu wa Mwadui FC aliliambia Mwanaspoti kuwa ''si kwamba timu yetu ni mbaya tumesajili ila hatupati matokeo mazuri kutokana na sababu mbalimbali, tumesikia taarifa za Julio ila tunasubili atuletee kwa maandishi nasi tutabariki kuondoka kwake hatuwezi pingana na uamuzi wake ambao yeye anauona wa busara.''   

''Kuna makocha wengi ambao wapo na wanatafuta kazi, hivyo akileta barua rasmi ya kuacha kazi basi hapo tutatafuta kocha mwingine atakayesaidiana na Khalid,  huyu atakuwa na muda maana mechi zimebaki nyingi lakini baadaye tutatafuta kocha mkuu,'' alisema Kilao. 

Julio aliipandisha timu hiyo daraja anaiacha na pointi tano katika mechi saba walizocheza kwa msimu huu, Mwadui imekuwa na mwenendo mbovu msimu huu tofauti na msimu wao wa kwanza ambayo ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kucheza Ligi kuu Bara. 

No comments:

Post a Comment