Rais wa Fifa Gianni Infantino ameshauri juu ya kuongezeka kwa timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia kufikia 48 ikiwa ni mojawapo ya ahadi yake aliyoitoa alipokuwa akiwania nafasi hiyo.
Muitaliano huyo ameshauri kwamba timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa, na kisha timu 32 kubaki zitaendelea katika hatua ya makundi baada ya mtoano kukamilika.
Moja ya ahadi zake ilikuwa kuongezeka kwa timu kufikia 40.
''Haya ni mawazo ya kupata ufumbuzi wa uhakika, tutayajadili mwezi huu na kuamua kila kitu 2017,'' alisema Infantino mwenye umri wa miaka 46.
Infantino aliingia madarakani na kuliongoza shirikisho hilo la Fifa February mwaka huu baada ya kujiuzulu Sepp Blatter.
''Wazo la Fifa ni kuendeleza soka katika dunia nzima, na Kombe la Dunia ni tukio kubwa. Ni zaidi ya ushindani ni tukio la jamii.
No comments:
Post a Comment