Sunday, October 16, 2016

PEP KUREJEA NOU CAMP JUMATANO IJAYO.

Pep Guardiola

Jumatano ijayo Pep Guardiola anarudi nyumbani Nou Camp kama mopinzani dhidi ya Barcelona, timu ambayo aliwahi kuichezea na kuwa kocha na kuipa mafanikio makubwa timu hiyo. Man City watakuwa wageni kwa Barca kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

Baada ya ushindi wake hapo jana dhidi ya Deportivo, Barcelona wataisubili Man City kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Jumatano ijayo City ambayo imepata sare ya 1-1 dhidi ya Everton hapo jana kwenye mchezo wa Premier League.

Man City watasafiri mpaka No Camp kwa ajili ya mchezo wa makundi Jumatano hii na utarudiwa Novemba 1 kwenye dimba la Etihad.
 
Memba wa MSN, Messi na Neymar akikosekana Suarez.
Matokeo ya jana kwa Barca yanawaweka sehemu nzuri kuelekea mchezo huo huku wakiwa tayali safu yao ya MSN kukamilika baada ya Lionel Messi kuweza kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua. 
 
Vicent Kompany katikati.
Huku kocha wa City Pep Guardiola akiomba mlinzi wake Vicent Kompany aweze kurejea uwanjani kwa ajili ya mchezo huo wa Jumatano ili kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa timu yake dhidi ya Barca ambayo aliwahi kuifundisha. 

No comments:

Post a Comment