Sunday, October 16, 2016

YANGA NA AZAM HAMNA MBABE, BOCCO AKABIDHIWA ZAWADI YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI.

Katibu Mkuu wa TFF Boniface Wambura akimkabidhi John Bocco zawadi yake.
Leo Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea kwa mchezo uliosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wadau mbali mbali wa soka nchini kati ya timu ya Yanga na Azam FC za jijini Dar es Salaam ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kwa miamba hiyo.
 Huku mchezaji nyota wa Azam John Bocco akipewa zawadi ya mchezaji bora wa mwezi Agosti uwanjani hapo baada ya kuonyesha kiwango kizuri mwezi uliopita. 

Akiwashinda wenzie wawili alioingia nao hatua ya mwishoni Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu, Bocco amezawadiwa kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment