![]() |
| Pique na Costa wakifurahia kwenye mechi yao ya taifa |
Mchezaji wa kimataifa wa Hispania Gerard Pique ameweka wazi kwamba baada ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia atastaafu kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo.
Pique aliyasema hayo baada ya kuwepo shutuma mbalimbali dhidi yake na yeye ameamua bora kuachana na La Roja baada ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.
Licha ya umri wake wa miaka 31 Pique ni mmoja wa mabeki imara na bora kwa Hispania, kwa kuweka msimamo wake kabla ya kumalizika mzunguko wa Kimataifa ameweka mtazamo wake na ueleweke mapema.
''2018 Kombe la Dunia nchini Russia ndio utakuwa mwisho wangu kuichezea timu ya taifa ya Hispania.'' Nimefikiria hilo kwa kina kuhusu hilo.

No comments:
Post a Comment