![]() |
| Pogba akifunga bao lake la kwanza kwa penati. |
Paul Pogba mchezaji ghali zaidi
duniani jana alithibitisha thamani yake kwa kuweza kuisadia timu yake ya Manchester United kuibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Fenerbance katika kundi A,alifunga goli la kwanza kwa penalti baada ya Juan Mata
kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kisha baadaye kuandika bao la pili
baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Jesse Lingard.
Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia
ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho
likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.
Robin
Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi
lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani
Sir Alex Ferguson.
Matokeo mengine katika michezo ya ligi ya Europa
THURSDAY 20TH OCTOBER 2016
FC Steaua București 1-1 FC Zürich
FK Krasnodar 0- 1 Schalke
FC Slovan Liberec 1-3 Fiorentina
Hapoel Be'er Sheva 0-1 Sparta Prague
Inter Milan 1-0Southampton
Osmanlispor 2-2 Villarreal
FK Qarabag 2-0 PAOK Salonika
Celta Vigo 2-2 Ajax
Standard Liege 2-2 Panathinaikos
Konyaspor 1-1 Sporting Braga
Shakhtar Donetsk 5-0 KAA Gent
FC RB Salzb 0-1 Nice

No comments:
Post a Comment