Luis Suarez anapokea pongezi nyingi kutoka kwa watunmbalimbali lakini hamna aliyetarajia kama atapokea kutoka kwa Patrice Evra ambaye walipishna kishwahili kipindi wako kwenye ligi ya Uingereza Premier League, kwenye mechi ya Oktoba 2011 Liverpool na Manchester United ambapo Surez alitoa maneno ya kibaguzi yaliyompelekea kufungiwa miezi 8 na kutozwa faini ya paundi 40,000 alipopatikana na hatia kabla ya kujiunga na Barcelona.
Suarez ambaye alijilikana na aina yake ya ukorofi wa mara kwa mara dhidi ya wachezaji wenzake alijiunga na Barcelona ambao walionekana kumdhibiti na kuweza kuwa na kiwango kizuri. Kiwango ambacho kimemng'arisha na kuweza kushinda kiatu cha dhahabu alichokabidhiwa jana kwa kufunga mabao mengi LaLiga msimu uliopita.
Hali hiyo ilipelekea Suarez kugoma kumpa mkono Evra kwenye moja ya mechi yao wakiwa Uingereza kati ya Liver na Man U.
Lakini Evra ameonyesha kwamba ameshasahau yote yaliyotokea kati yao na kumuandikia ujumbe uliosomeka-
"Siku zote ni upendo na sio chuki milele, wewe ni mchezaji mzuri na namba 9 bora Hongera Luis. Nupenda huu mchezo.!!!



No comments:
Post a Comment