
Kocha wa timu ya taifa ya Colombia Jose Pekerman anaamini timu yake ilistahili ushindi uliopata wa 1-0 dhidi ya Paraguay hapo jana kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
Bao la dakika 91 la Edwin Cadona ambaye akitokea benchi lilifanya timu hiyo kutoka kifua mbele ya Paraguay kwenye mchezo huo. Licha ya kuhitaji bao la dakika za lala salama kocha huyo ananmini kuwa kikosi chake kilicheza vizuri na kilistahili pointi tatu.
''Tulikuwa na wasiwasi kuelekea mchezo huu,'' aliwaambia waandishi wa habari.
''Lakini nadhani matokeo ni ya haki. tumejifunza kuzuia na kushambulia.''
Kocha huyo ambaye alisifia eneo lake la ulinzi wakati Colombia ikishinda michezo mitano katika mechi tisa za kufuzu.
''Mchakato haukuwa rahisi,'' alisema Muargentina huyo.
''Timu zote zilikuwa na ulinzi na tulitengeneza nafasi chache.''
No comments:
Post a Comment