Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya leo hii pia kuendelelza rekodi yake ya kutopoteza mechi kwa kuifunga Stand United ya Shinyanga.
Kwa sasa Simba SC imefikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 za mechi 14.
Bao
hilo lilifungwa na winga machachari wa Wekundu hao wa Msimbazi, Shizza
Ramadhani Kichuya kwa penalti dakika ya 33 baada ya mshambuliaji Mrundi,
Laudit Mavugo kuangushwa na beki Adeyum Ahmed kwenye boksi.
Huko Mbeya nako Yanga ikiwa mgeni imeshindwa kufurukuta mbelel ya Mbeya City baada ya kukubali kipigo cha cha bao 2-1 kutoka kwa City kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine. Beki wa kushoto Hassan Mwasapili aliweza kuifungia timu yake bao dakika ya sita na Kenny Ally akaifungia timu yake bao la pili dakika ya 36 kabla ya Donald Ngoma wa Yanga kusawazisha ndani ya dakika ya 45 lakini mpaka mpira unaisha matokeo yakawa hivyo hivyo.
No comments:
Post a Comment