Hatimaye mchezaji raia wa Ivory Coast Yaya Toure anayechezea Manchester City ameweza kuomba msamaha kwa kocha wake Pep Guardiola ambaye kwa muda walikuwa hawana mawasiliano mazuri hali iliyopelekea wakala wa mchezji huyo kuingilia kati na kupelekea hali tete kwa kocha wa klabu hiyo.
Toure ambaye aliachwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest kwenye raundi ya pili hali iliyopeleka wakala wake Dimitri Seluk kuingilia kati na kutupiana maneno na kocha Pep Guardiola ambaye baadae akataka aombwe msamaha ili aweze kumjumuisha mchezaji huyo kikosini.
Dimitri alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata uhamisho wa Toure kutoka Barcelona ambao Pep alihusika kuwa haukuwa na haki kwa mchezaji huyo mwaka 2010.
Toure ambaye ametumia mtandao wa Facebook kuomba radhi huku kukiwa hakuna jina la Guardiola au Seluk lililotajwa.
''Natamani kuomba msamaha kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha kwenye uongozi wa klabu kwa kutokuelewana kwa yaliyopita,'' alisema Toure.
''Taarifa hiyo haiusiani na maoni yangu ndani ya klabu au wau wanaofanya kazi hapo. Sina chochote zaidi ya heshima na Manchester City na kuitakia yaliyo bora klabu.
''Nina furaha kuwa mchezaji atakaye kuwa sehemu ya historia ya klabu na ninahitaji kuisaidia City kufanikiwa zaidi. Ninapenda kucheza soka na kuwafurahisha mashabiki.
''Kwa walaka huu
No comments:
Post a Comment