Klabu ya Arsenal hapo jana imeweza kufuzu raundi ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakitokea nyuma baada ya kuilaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa mabao 3-2 mabao ya Xhaka , Groud na Ozil yaliweza kuifanya Arseanal kutinga 16 bora. Mesut Ozil alifunga bao la dakika za
mwisho na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma 2-0 na kulaza Ludogorets
Razgrad ya Bulgaria na kuwafikisha hatua ya mondoano Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya.
Arsenal sasa wamefika hatua ya 16 bora na wameendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.
Matokeo mengine ya mechi za jana ni kama ifuatavyo-
KUNDI A
Basel 1-2 Paris Saint Germain
Ludo Razgd 2-3 Arsenal
KUNDI B
Besiktas 1-1 Napoli
Benfica 1-0 Dynamo Kiev
KUNDI C
Bor Monchengladbach 1-1 Celtic
Manchester City 3-1 Barcelona
KUNDI D
Atletico Madrid 2-1 FC Rostov
PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich
No comments:
Post a Comment