![]() | |
MSN wakishangilia bao. |
Wakati mechi ikiendelea katika dimba la Etihad jijini Manchester Uingereza Lionel Messi anafunga bao ambalo linafanya avunje rekodi ya nyota Mhispania Raul Gonzalez kwenye Ligi ya Mabingwa. Raul ambaye kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa aliweza kufunga mara 53 kwa Real Madri na Schalke 04 katika magoli yake 71 kwenye miaka 16 idadi ambayo Messi ameifikia.
Messi kwa sasa amefikisha magoli 90 nyuma ya Cristiano Ronaldo mwenye magoli 95 kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Kwenye mchezo huo Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 5-3 kufuatia kupigwa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza.
Messi alikuwa wa kwanza kuifungia Barca dakika ya 21 kabla ya Gundogan kusawazisha bao hilo dakika ya 39 na De Bryune kufunga bao la pili dakika ya 51 na Gundogan tena dakika ya 74 kukamilisha kalamu hiyo ya mabao.
No comments:
Post a Comment