Chama cha Soka Argentina AFA kimetuma barua ya kuomba msamaha kwa klabu ya Barcelona baada ya kocha wa taifa ya Argentina Edgardo Bauza kuikosoa juu ya uangalizi wa afya ya Lionel Messi ambaye aliumia kwenye mchezo wa Ligi akiwa na Barca dhidi ya Atletico Madrid ambapo nyota huyo alitolewa kipindi cha pili cha mchezo baada ya kupata maumivu ya msuli wa kinena kwenye mguu wake wa kulia.
Na baada ya hapo kocha wa Argentina aliishutumu vikali klabu hiyo kwa kusema kwamba hawamjali nyota huyo na kuwapa wao timu ya taifa kumuhudumia kipindi hiki cha majeruhi, kitu ambacho watu wengi walikipinga juu ya kauli ya kocha huyo juu ya Barca kushindwa kumuhudumia Messi.
Na Barcelona baada ya kupokea ombi hilo wamethibitisha kumsamehe kocha huyo.
Msemaji wa Barcelona Josep Vives alisema kwamba AFA wamekiri kuwa maneno ya kocha huyo wa La Albiceleste yalikuwa ya bahati mbaya na hayakuwa na nia ya kusababisha madhara.
''Wote kwa pamoja, AFA na Barcelona tunaangalia upya na kuungana jinsi ya kumsadia Messi kupona haraka.'' Vives aliiambia Barca Tv.
Messi ambaye atakuwa nj'e kwa wiki kadhaa, kumekuwa na tetesi kuwa The Catalans hawataki kumpa ruhusa mshambuliaji mwenzake Luis Suarez kwenda kwenye mechi za timu ya taifa za kufuzu kwa kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kuchezwa mapema mwezi Oktoba.
Msemaji huyo alipingana na tetesi hizo na kuzikataa.
''Huo ni uwongo.''
''kama Uruguay watamwita Suarez na kama yuko fiti basi ataenda na atacheza mech zote dhidi ya Venezuela na Colombia.

No comments:
Post a Comment