Monday, September 26, 2016

BORRUSIA DORTMUND WAIKEJELI MADRID JUU YA JEZI RANGI ZA NJANO


Ni kama vile kuamsha presha ya mchezo wao kwenye Champions League dhidi ya Real Madrid, Borrusia Dortmund wameikejeli timu hiyo juu ya timu zilizokutana nazo na kutoka nazo sare, zote zilivalia jezi za njano na kuwaambia zinawapa homa ya manjano.

Madrid ambao walilazimishwa sare dhidi yao na Villarreal na Las Palmas. 

''Una wakati mgumu ukicheza dhidi ya timu zinazovalia njano, wewe kweli ni Real Madrid.''Borrusia waliposti kupitia akaunti yao ya kijamii ya Twitter 

''Real Madrid wana wakati mgumu pia na kijani,'' Sporting walijibu kwenye Twitter hiyo. Bahati njema kwa wote.  

Miamba hiyo miwili inakutana  Jumanne hii Septemba 27 Madrid ikiwa mgeni kwenye mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Signal-Iduna Park.

No comments:

Post a Comment