Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani Lukas Podolski amemkosoa kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwa kitendo chake cha kutomtumia Bastian Schweinsteiger.
Kiungo huyo mzoefu alijiunga na United akitokea Bayern Munich msimu wa 2015/2016, na toka awe majeruhi amekuwa na kazi ya ziada kurudi tena Old Trafford chini ya kocha huyo.
Mourinho ambaye aliamua haraka kuwa hamuitaji kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, na kumuweka katika wachezaji wa akiba kitendo ambacho kinamuuma Podolski ambaye alikuwa ni mchezaji mwenzake katika timu ya taifa ya Ujerumani.
''Wakati ukiangalia kazi aliyonayo Bastian, naweza kusema tu kwamba kile kinachotokea sio sahihi kwa mchezji wa kiwango chake,'' Podolski aliiambia Bild.
''Sijui kile Mourinho alichojadili na Bastian, Lakini ukweli ni kwamba haiko sawa kumuacha mtu kama Bastian kuwa wa akiba.
''Kocha siku zote anatakiwa kufungua milango kwa wachezaji wake wote, na haswa kwa mchezaji kama Bastian.''
Shweinsteiger ana mkataba na United mpaka June 2018.

No comments:
Post a Comment