Thursday, September 22, 2016
MESSI ATARAJIWA KURUDI UWANJANI DHIDI YA MANCHESTER CITY CHAMPIONS LEAGUE.
Mshambuliaji Lionel Messi ambae atakuwa nj'e kwa takribani wiki tatu baada ya hapo jana kupata majeraha katika mechi ya Barcelona na Atletico Madrid ambayo walitoka sare ya 1-1.
Lionel Messi ataweka vituko vyake kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Manchester City katika Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano Oktoba 19, kama alama yake ya kurejea kwake uwanjani.
Messi ambaye atakosa michezo mitatu ya Barcelona inayofatia, dhidi ya Sporting Gijon, Borrusia Monchengladbach na Celta Vigo na miwili kwa Albiceleste dhidi ya Peru na Paraguay.
Luis Enrique anatarajia kumchezesha nyota huyo katika mchezo wao na Depotivo ili kuweza kuona kama nyota huyo amepona na kuwa tayari kwa kiwango cha juu kabla ya kupambana katika mechi itayofata.
Kwa maumivu yake ya misuli kwenye kinena mguu wake wa kulia, Messi anakuwa mchezaji wa sita wa Barcelona msimu huu kuwa na matatizo ya misuli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment