Sunday, September 4, 2016
ANCELOTTI SIWEZI KUZIFUNDISHA ATLETICO MADRID AU BARCELONA
Ancelotti amesisitiza kuwa hawezi kuja kuzifundisha timu za A.Madrid au Barcelona kwa heshima ya Real Madrid kutokana na upinzani baina ya timu hizo za La liga. Kocha huyo ambae sasa anaifundisha Bayern Munich ya Ujerumani alitumia miaka miwili kuifundisha Real Madrid huku ikiifunga Atletico Madrid kwenye fainali ya ligi ya mabingwa 2014, ''Ancelotti anaamini kuwa ikitokea kurudi kwake Hispania basi itakuwa Santiago bernabeu na sio kwa wapinzani wao.
''Hapana siwezi kuzifundisha (At.Madrid au Barca) muitaliano huyo alisema hayo kweye mahojiano na marca ''naheshimu heshima niliyoipata Real Marid na pia sitoweza kuzifundisha Lazio au Inter'''
Nina ziheshimu timu zote hizo lakini siwezi kuzifundisha sababu tayali nilishakuwa kocha wa Real Madrid kwa miaka miwili. Kocha huyo ataiongoza timu yake ya sasa ya Bayern Munich dhidi ya Atletico Madrid September 28 kwenye uwanja wa Vicente Caldecon baada ya droo kuwaweka pamoja kwenye hatua ya makundi ligi ya mabingwa Ulaya. Aliongeza pia kwa kusema ''kuwa mapokez hayatabiriki baina ya timu pinzani na kocha mpinzani'' nitafanya kazi yangu kwa ajili ya ushindi kwa timu yangu kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye uwanja wenye changamoto wa Caldecon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment